Kikosi cha Yanga |
Kikosi cha Gor-Mahia |
Mchezaji wa Yanga, Amis Tambwe akiwa chini huku wachezaji Collins Okoth (kulia) na Harun Shakava (kushoto) wa Gor Mahia ya Kenya wakiwania mpira wakati wa mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Kagame uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. Yanga imefungwa mabao 2-1. |
Mashabiki wa Yanga |
WENYEJI Yanga wameanza
vibaya kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la
Kagame, baada ya kufungwa mabao 2-1 na Gor Mahia ya Kenya katika mchezo wa
Kundi A kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kipigo cha Yanga kwa kiasi kikubwa kilichangiwa na kucheza
pungufu kwa zaidi ya dakika 65, kutokana na mshambuliaji wake, Donald Ngoma
raia wa Zimbabwe, kutolewa kwa kadi nyekundu mapema kipindi cha kwanza.
Yanga waliuanza vizuri mchezo huo na kufanikiwa kupata bao
la kuongoza dakika ya tano tu kupitia kwa Ngoma aliyepiga mpira mrefu kama
krosi kutoka upande wa kushoto na kutinga nyavuni.
Bao hilo halikudumu sana, kwani Gor Mahia walifanikiwa
kusawazisha dakika ya 18 kupitia kwa na Dirkir Glay aliyepiga shuti kali la
mpira wa adhabu lililomshinda kipa Ally Mustafa ‘Barthez’.
Faulo hiyo ilitolewa baada ya beki wa kulia, Juma Abdul
kumuangusha Godfrey Walusimbi nje ya boksi.
Mwamuzi Ssali Mashood alimtoa nje kwa kadi nyekundu Ngoma
baada ya kumuonesha kadi ya pili ya njano kutokana na kumsukuma Shakava wa Gor baada ya kumpamia na
mpira hadi nje ya uwanja dakika ya 25.
Kipindi cha pili, Gor Mahia waliingia na mashambulizi ya
kulazimisha na kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya kwanza tu kupitia kwa
mshambuliaji wake, Michael Olunga, aliyewapiga chenga mabeki wa Yanga kabla ya
kufunga.
Yanga walipoteza nafasi nzuri ya kupata sare dakika ya 73,
baada ya nahodha wake, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kukosa penalti baada ya shuti
lake kudakwa kiurahisi na golikipa.
Katika mchezo huo uliohudhuriwa na Waziri Mkuu wa zamani wa
Kenya, Raila Odinga, kwa ujumla Yanga SC iliathiriwa na kucheza pungufu.
Yanga: Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul/Joseph Zuttah dk
75, Mwinyi Hajji Mngwali, Kevin Yondani, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mbuyu Twite,
Simon Msuva/Kpah Sherman dk 69, Haruna Niyonzima, Amisi Tambwe, Donald Ngoma na
Deus Kaseke/Salum Telela dk 84.
Gor Mahia: Boniface Olouch, Mussa Mohammed, Sibomana Abouba,
Harun Shakava, Kari Nzigiyimana, Dirkir Glay, Khalid Aucho/Erick Ochieng dk 89,
Godfrey Walusimbi/Ronald Omino dk 86, Innocent Wafula/Enock Agwanda dk86, Medie
Kagere na Michael Olunga.
Katika mchezo wa awali, APR ya Rwanda ilianza vyema michuano hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Al Shandy ya Sudan, huku
Katika mchezo wa awali, APR ya Rwanda ilianza vyema michuano hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Al Shandy ya Sudan, huku
Katika mchezo huo wa Kundi C, bao pekee la APR lilifungwa na
kiungo Bizimana Djihad, dakika ya 64 kwa shuti kali kwa kupasua katikati ya
uwanja na baada ya kupata upenyo.
Kiungo huyo aliyesajiliwa mapema mwezi huu kutoka kwa
mahasimu, Rayon Sport ili kuziba pengo la Jean Baptiste Mugiraneza aliyehamia
Azam FC, ni mtoto wa dada wa kiungo wa Yanga SC, Haruna Niyonzima, ambaye pia
aliwika Rayon na APR kabla ya kuja Tanzania.
No comments:
Post a Comment