Waziriwa wa Utamaduni, Vijana na
Michezo wa Sudani Kusini Mh. Stephen Lado Onesimo jana aliitembelea timu
ya Malakia FC wakati ikifanya mazoezi kwenye uwanja wa Karume wakati
ikijiandaa kwa ajili ya mchezo wake wa leo dhidi ya KCCA ya Uganda
mchezo utakaopigwa majira ya saa 8:00 mchana kwenye uwanja wa Taifa
ikiwa ni mwendelezo wa mashindano ya Kagame Cup hatua ya makundi.
Waziri huyo amesema, wachezi wa
Malakia wanahitaji kushinda mchezo huo japo tayari wananafasi ya kucheza
hatua ya robo fainali lakini ushindi kwenye mchezo huo utazidi
kuwajengea heshima kwenye soka la ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati
lakini pia watakuwa wanaweka heshima ya nchi yao (Sudan Kusini) ambayo
imekuwa ikibezwa kwenye soka tangu ijitenge kutoka Sudan (Kaskazini).
Mchezo
wenu dhidi ya KCCA ni muhimu sana ndiyo maana nimekuja hapa kuzungumza
na ninyi ili kuhakikisha mnashinda mchezo huo na kujiwekea heshima
nyinyi wachezaji na klabu yenu lakini kubwa zaidi ni nchi yetu ya Sudan
ambayo imekuwa ikibezwa kwenye michezo hasa soka tangu tujitenge kutoka
Sudan”, alizungumza kwa hisia.
“Nitakuwepo
pia uwanjani kuwashuhudia mkicheza mchezo wenu, nahitaji mjitume kwa
ajili ya nchi yetu ya Sudan na endapo mtashinda mchezo wenu, nawaahidi
kuwapa zawadi. Nimezungumza na kocha wenu ameniambia tayari mnanafasi ya
kucheza robo fainali ya mashindano haya, lakini mimi nahitaji mshinde
mchezo huu ili mkacheze robo fainali mkiwa mnaheshimiwa”, alisisitiza.
“Nidhamu kwenye mchezo ni kitu
muhimu sana, kila mtu anatakiwa awe na nidhamu ya hali ya juu wakati wa
mchezo, muelekezane wenyewe kwa wenyewe muwapo uwanjani nani anatakiwa
kufanya nini ili kumpunguzia kazi kocha wenu. Mimi nawatakia kila kheri
na ninaimani na ninyi na ninamatumaini tutashinda mbele ya KCCA”,
alimaliza.
Malakia
ilishinda mchezo wake wa kwanza mbele ya Adama City lakini ikapoteza
mchez wake wa pili dhidi ya Azam FC, leo inaingia uwanjani kuikabili
KCCA hata kama itapoteza mchezo wa leo itaingia kucheza robo fainali ya
Kagame kama best loser. Mchezo mwingine wa kundi hilo (Kundi C) utakuwa
ni kati ya Azam FC dhidi ya Adama City utakaochezwa kuanzia saa 10:00
jioni kwenye uwanja wa Taifa.
No comments:
Post a Comment