Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, July 4, 2015

SIMBA HAOOO LUSHOTO KWA WIKI MBILI







SIMBA itaondoka jijini kesho alfajiri kwenda kuweka kambi kwenye safu za milima ya Lushoto mkoani Tanga kwa ajili ya kujiandaa na Ligi Kuu ya Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza Agosti 22.
Akizungumza baada ya mazoezi yaliyofanyika kwenye Ufukwe wa Coco, jana, Kocha Mkuu wa Simba, Dylan Kerr alisema wanakwenda kuweka kambi kwa wiki mbili Lushoto kwa sababu ya hali ya huko ni nzuri kwa mazoezi.
“Kwa sababu hali ya hewa ya Lushoto ni baridi itafanya wachezaji wafanye mazoezi sana kuliko hali ya hewa ya joto pia itasaidia kocha wa fitness, Dusan kujua stamina (fitness)  ya kila mchezaji na saikolojia”, alisema Kerr.
Pia Kerr alisema anafurahi kwa sababu muitikio wa wachezaji ni mzuri  japo amepata taarifa kuwa kuna wengine ambao wapo kwenye mfungo wa Ramadhan lakini hakuna tofauti kati yao.
Kerr alisema baada ya kambi ya Lushoto ataomba apate mechi tano za kirafiki ili apime stamina (fitness) na kile ambacho amefundisha kwa wiki tatu
Wachezaji watakaondoka ni kipa Ivo Mapunda ambaye ni chaguo la kocha wa makipa, Idd Abdul ambaye amemalizana na uongozi juzi kutokana na pendekezo la kocha huyo kwani uongozi ulikuwa unasusua umsajili nani kati ya Ivo na Kaseja.
Wengine ni kipa Peter Manyika,  Denis Richard, Samir Nuhu, Mohamed Fakhi, Murushid Juuko, Peter Mwalyaje, Musa Hassan ‘Mgosi’, Elias Maguri, Awadh Juma, Ibrahim Ajib na Emanuel Alex ambaye anafanya majaribio akitokea Afrika Kusini katika klabu ya Olmpio inayoshiriki ligi daraja la pili.
Pia wapo Issa Abdallah, Said Issa Mbaraka Yusuf na David Kisu ambao wamepandishwa kutoka kwenye timu B.

No comments:

Post a Comment