Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, July 14, 2015

MAKAMU MWENYEKITI WA BODI YA LIGI, SAID MOHAMED AFUNGUA KOZI YA MAKOCHA WA MAKIPA


Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Salum Madadi (kushoto) akimtambulisha Mkufunzi wa FIFA Elaxander kutoka Ufaransa (wa pili toka kushoto) wakati wa ufunguzi wa kozi ya makocha wa magolikipa inayoendelea katika Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam jana. Wa pili toka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu nchini, Said Mohamed na kulia ni Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa


Mkufunzi wa FIFA Elaxander kutoka Ufaransa (aliye katikati ya waliosimama) kwa pamoja na washiriki  wa kozi ya makocha wa golikipa inayoendelea katika Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam


MAKAMU Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi nchini, Said Mohamed amewataka washiriki wa kozi ya makipa kutumia vizuri mafunzo watakayopata katika kuendeleza mpira nchini.

Said Mohamed ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya utendaji ya TFF, aliyasema hayo jana wakati akifungua kozi ya makocha wa golikipa inayoendelea katika Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.

“Naishukuru FIFA kwa kuipa Tanzania nafasi ya kuendesha mafunzo hayo ya makocha wa makipa kwa mara ya kwanza nchini pia nawaomba washiriki wa kozi hii mtumie vema nafasi kwa ajili ya kuendeleza mpira wa miguu”, alisema Said

Naye mshiriki Mohamed Mwameja ‘Tanzania One’ ambaye amewahi kuidakia Simba na timu ya Taifa alishukuru kupata kozi hiyo na kusema itawasaidia kujua makosa yao kwani wamekuwa wakifundisha kwa uzoefu ambao waliupata wakati wakicheza.

“Sisi tunafundisha kwa kutumia uzoefu tuliopata kutoka kwa waliotufundisha wakati tukicheza hivyo kozi hii itatufanya tujitambue wapi tulikuwa tukikosea ili turekebishe na tupate makipa bora”, alisema Mwameja

 Jumla ya makocha 31 wanashiriki kozi hiyo kutoka vilabu vyote viliyovopo Ligi Kuu ya Tanzania Bara na Zanzibar na magolikipa wa zamani walio wahi kudaka timu za Taifa.

Kozi hiyo inaendeshwa na mkufunzi wa FIFA Elaxander kutoka nchini Ufaransa, ambaye alidumu kama golikipa kwa miaka 20 na inatarajiwa kufungwa Julai 17, mwaka huu 

No comments:

Post a Comment