KIINGILIO
kwenye michezo ya Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup) katika
hatua ya nusu fainali ni shilingi elfu tatu (3,000).
Akizungumza
na wandishi wa habari jana, Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, Baraka
Kizuguto alisema kuwa kiingilio hivyo vinaendana na hatua yenye
“Viingilio
vya michezo ya kesho (leo) ni VIP
A ni 15,000 na VIP B & C,
10,000 na sehemu nyingine ya
uwanja iliyobakia ni 3,000 kwa viti vya rangi ya bluu, kijani na rangi ya
chungwa”, alisema Kizuguto.
Timu
nne kutoka katika nchi nne wanachama wa michuano hiyo, Azam FC (Tanzania), Gor
Mahia (Kenya), KCCA (Uganda) na Al Khartoum (Sudan) zimefuzu kwa hatua ya nusu
fainali itayochezwa uwanja wa Taifa leo
Mchezo
wa kwanza utakaonza saa 7:30 mchana utazikutanisha timu za Gor Mahia ya Kenya
itakayocheza dhidi ya Khartoum ya Sudan, mchezo unaotarajiwa kuwa wa vuta
nikuvute kufutia timu hizo kutoka sare katika mchezo wake wa awali hatua ya
makundi.
Katika
mchezo wa kwanza uliozikutanisha timu hizo, kocha wa Khartoum Kwesi Appiah na
Frank Nuttal wa Gor Mahia walitoka sare ya bao 1- 1 ndani ya dakika 90, hali
ambayo inapelekea kufaya mchezo kuwa mgumu kwa kila timu kuhitaji nafasi ya
kusonga mbele hatua ya fainali.
Gor
Mahia mabingwa mara tano wa michuano hiyo, wataingia uwanjani kusaka ushindi
ili kusonga hatua ya fainali ili waweza kutwaa ubingwa huo kwa mara ya sita,
sawa na klabu ya Simba inayoongoza kwa kutwaa ubingwa huo.
Kocha
Frank Nuttal atakua akiwategemea wachezaji wake nyota, Khalid Alucho, Kagere
Meddie, Michael Olunga, Sibomana Abouba, Karim Nzigiyimana, Godfrey Walusimbi,
Nahodha Musa Mohamed, na mlinda mlango Boniface Oluoch katika kusaka ushindi
dhidi ya Khartoum.
Kwesi
Appiah atashuka dimbani akiwategemea wachezaji wake nyota, Antony Akumu,
Dominic Abdui, Samawal Meshani, Wagdi Wawd, Ouismaila Baba na nahodha Amin
Ibrahim.
Vita
kali itakua kwa washambulaji Michael Olunga wa Gor Mahia na Salaheldin Osman
wote wenye mabao manne, wakiwania kuongeza bao katika mchezo huo wa kesho ili kujiweka
katika mazingira mazuri ya kutwaa kiatu cha dhahabu.
Nusu
fainali ya pili itawakutanisha Azam FC dhidi ya Mamlaka ya jiji la
Kampala (KCCA), mchezo utaokanza majira ya 9:45 kwa saa za Afrika na Kati
katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mchezo
huo pia unatarajiwa kuwa na upinzani mkali kufutia timu hizo katika mchezo wa
hatua ya makundi, Azam FC kuibuka na ushindi wa bao 1- 0, bao liliofungwa na
nahodha wake John Bocco.
KCCA
chini ya kocha wake Mike Mutebi watashuka dimbani kusaka ushindi katika mchezo
huo, ikiwa ni kulipiza kisasi kwa mchezo wa kwanza na kupata ushindi
utakaowavusha mpaka katika hatua ya fainali.
Kocha
Mutebi atakuwa akiwategmea wachezaji wake nyota, Nahodha Tom Matiko, Opio
Emmanuel, Joseph Ochaya, Hassan Waswa, Isaac Sserenkuma, Habib Kavuma na
Muzamil Mutyaba.
Azam
FC itashuka dimbani kutaka kuendeleza ubabe wake dhidi ya KCCA ya Uganda, na
kuweza kukata tiketi ya kucheza fainali siku ya jumapili katika uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam.
Kocha
wa Stewart Hall wa Azam atakua akijivunia safu yake ya ulinzi ambayo
haijaruhusu bao tangu kuanza kwa michuano hiyo, huku safu yake ya ushambuliaji
ikiwa imefunga mabao 8 katika michezo mine iliyocheza.
Hall
atashuka dimbani akiwategemea nyota wake Nahodha John Bocco, Pascal Wawa, Aggrey
Morris, Himid Mao, Kipre Tchetche, Jean Baptist Mugiranenza, Frank Domayo na
mlinda mlango Aishi Manula.
No comments:
Post a Comment