Timu ya Al Shandy kutoka
nchini Sudan, Al Malakia kutoka Sudan Kusini na KMKM kutoka Visiwani Zanzibar
zinatarajiwa kuwasili kesho jijini Dar es salaam tayari kwa ushiriki wao kwenye
michuano ya kombe la Kagame.
Al Shandy wanatarajiwa
kuwasili kesho Alhamisi saa 3 kamili asubuhi kwa usafiri wa shirika la Ndega la
Kenya (KQ), KMKM wakitarajiwa kuwasili majiraa ya saa 5 kamili asubuhi kwa boti
ya Kilimanjaro, na Al Malakia wakitarajiwa kuwasili saa 10 jioni kwa ndege ya
Rwanda Air.
Viwanja vya mazoezi
vitakavyotumika kwa timu zinazoshiriki michuano ha Kagame ni Chuo cha Ualimu
(Duce), TCC – Chang’ombe, Sekondari ya Loyola, Bora Kijitonyama, Polisi
Kurasini, Chamazi, Uwanja wa Uhuru.
Timu 11 zitafikia katika
hoteli za Durban (Mnazi Mmoja), Chichi (Kinondoni) Ndekha, Grand Villa,
Travertine (Magomeni), wakati wenyeji Azam na Yanga watakua na kambi zao kwa
ajili ya mashindano hayo.
Wasifu wa Al Khartoum:
Al Khartoum ni kati ya
wawakilishi wawili wa Sudan kwenye kombe la Kagame. Al Khartoum ni kiboko ya
vigogo katika Ligi ya Sudan kutokana na
kutoa upinzani mkali katika ligi ya nchi hiyo inayozijumuisha timu za Al Hilal,
El Merreikh na Al Shandy.
Wachezaji wa kuangaliwa:
Mshambuliaji Ismail Baba
ambaye ni mchezaji wa zamani wa Coton Sports ya nchini kwao, Kameruni
anategemewa kuongoza safu ya ushambuliaji ya timu hii kutoka jiji la Khartoum.
Kiungo mshambuliaji,
Dominic Aboy, raia wa Sudani Kusini anategemewa kuonesha ufundi katikati ya
dimba. Salah Al Amini ni mchezaji mwingine wa kutupiwa jicho.
Benchi la ufundi:
Katika kujaribu
kufurukuta kutoka kwenye ubabe wa timu mbili maarufu za Sudan, Al Merriekh na
Al Hilal, wawakilishi hawa wa Sudani walivuka mipaka na kumuajiri kocha wa
zamani wa timu ya Taifa ya Ghana, Kwesi Appiah.
Huu utakuwa mtihani wa
pili mkubwa kwa kocha Kwesi Appiah baada ya kushindwa kufurukuta kwenye
mashindano ya kombe la Shirikisho mbele ya Power Dynamos ya Zambia.
Kundi ililopo:
Al Khartoum iko kwenye
kundi A la michuano ya kombe la Kagame kwa mwaka huu ikijumuishwa pamoja na
Yanga, Gor Mahia ya Kenya, KMKM ya Zanzibar na Telecom ya Djibout.
Bila shaka ni kundi gumu
kwenye michuano ya mwaka huu.
Rekodi kombe la Kagame:
Al Khartoum ni wageni wa
mashindano haya. Rekodi ya kubwa nje ya Sudan, ni kufanikiwa kufika kwenye
hatua ya kumi na sita bora ya mashindano ya Kombe la shirikisho la CAF mnamo
mwaka 2011.
Wasifu wa
KMKM
Klabu ya KMKM itawaiwakilisha Tanzania kwa upande wa
Zanzibar kwenye michuano ya Kombe la Kagame inayotarajiwa kuanza Jumamosi
kwenye viwanja vya Taifa na ule wa Karume.
Historia ya KMKM kwenye
Kombe la Kagame:
Imeshiriki mara kadhaa bila
kushinda taji hili. Ushiriki wao haukuwa
mzuri kwenye michuano ya mwaka jana iliyofanyika jijini Kigali, Rwanda.
Hata hivyo, KMKM wameonesha
nia ya kufanya vizuri mwaka huu kwa kufanya maandalizi mapema.
Tayari wamecheza mechi tatu
mfululizo za kirafiki kama sehemu ya maandalizi yao ya kujaribu kufungua
ukurasa mpya wa kufanya vyema kwenye mashindano ya Kagame.
Benchi la Ufundi:
KMKM iko chini ya kocha
mzoefu Ali Bushiri.
Kiungo mshambuliaji, Juma
Bwawa, mshambuliaji Matheo Anthony na Hamisi Ally ni miongoni mwa wachezaji
wanaopewa nafasi ya kuisadia klabu hii. Wengine ni pamoja na mlinzi Khamisi
Ally, na Musa Saidi.
NB: Logo maalumu ya michuano
ya CECAFA KAGAME CUP 2015 imeambatanishwa, pamoja na wadhamini DTB Bank na AAR.
No comments:
Post a Comment