Baraza la Vyama Vya Soka kwa
Nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kesho Alhamis tarehe 16 Julai, 2015
litaendesha mtihani wa utimamu wa mwili (Pysical test) kwa waamuzi wa
watakochezesha michuano ya kombe la Kagame inayoanza mwishoni mwa wiki huu.
Zoezi hilo la utimamu kwa
waamuzi watakochezesha mashindano ya Kagame, litafanyika kuanzia saa 2 asubuhi
katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam litasimamiwa na kamati ya waamuzi
yay a CECAFA.
Waamuzi wanaotarajiwa kuhudhuria
zoezi hilo ni Ali Ahmed, Suleiman Bashir (Somalia), Ahmed Djama (Djibout),
Yetayew Belachew (Ethiopia), Kakunze Herve (Burundi), Davis Omweno, Peter
Sabata (Kenya), Issa Kagabo, Hakizimana Louis (Rwanda), Ahemd El Faith (Sudan),
Lee Okelo na Mashood Ssali (Uganda), Israel Mujuni na Ferdinand Chacha
(Tanzania).
No comments:
Post a Comment