WACHEZAJI
Simba wachekelea ujio wa kocha mpya Muingereza Dylan Kerr aliyewasili jana
tayari kuanza kazi ya kukinoa kikosi hicho kwa msimu ujao wa Ligi Kuu ya
Tanzania Bara.
Akizungumza
baada ya mazoezi yaliyofanyika kwenye gym ya Chang’ombe jijini Dar es Salaam,
Mussa Mgosi alisema wao wamefurahi kusikia kocha amekuja hivyo wapo tayari
kumpokea na kumpa ushirikiano.
“Sisi wachezaji
kazi yetu ni kucheza mpira hivyo kocha yeyote atakaye letwa tunampokea na
tunampa ushirikiano na leo tunalifikiri angekuja tusalimiane naye lakini ndo
hivyo hajafika ila tunamkaribisha sana’, alisema Mgosi
Kerr aliwasili
jana saa 10 jioni , Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na ndege ya Shirika la Emitares na kulakiwa na
wajumbe wawili wa kamati ya Simba, Collin Frisch na Said Tully na kuongea na
waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali waliokuwepo uwanjani.
Kerr amerithi
mikoba ya Mserbia Goran Kopunovic,
amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuifundisha Simba ambapo atakuwa
anasaidiwa na kiungo wa zamani wa timu hiyo Suleman Matola na kocha wa makipa
Idd Salim toka Kenya ambaye naye aliwasili juzi.
Simba
waliamua kuachana na Kopunovic na kusaka kocha huyo mpya baada ya Mserbia huyo
kuhitaji Simba imlipe kiasi cha Dola za Marekani 50,000 (sh. Milioni 100) kama
ada ya usajili na mshahara wake ambapo kila mwezi atakuwa analipwa dola za
Marekani 14,000 (sh. Milioni 28).
Baada ya
kushindwana kwenye malipo ndipo uongozi uliamua kumsaka kocha mpya na kumpata
Kerr ambaye inasemekana atalipwa mshahara wa dola za marekani 9,000 sawa na
milioni 18 kwa mwezi.
No comments:
Post a Comment