Kufuatia pendekezo la sekretariet ya TFF ambalo baadae lilipitishwa na
Mkutano Mkuu wa TFF kila mkoa unatakiwa kuwa na kituo chake cha kulea na
kukuza vipaji vya mpira wa vijana umri kuanzia miaka 8-17.
Kwa
mikoa ambayo tayari ina kituo ambacho inakiendesha yenyewe TFF inaonba
ipatiwe taarifa hiyo ikiwa ni pamoja na kufahamishwa jina la kituo, jina
la mwalimu na sifa zake na utaratibu wa mafunzo.
Kwa mikoa ambayo
haina kituo TFF inagiza mikoa hiyo kuingia ubia na kituo kimoja ambacho
tayari kina program ya kukuza na kuendeleza vipaji ili kijulikane kuwa
ni kituo maalum cha mkoa husika.
Katika hilo TFF inaagiza kamati ya
utendaji ya mkoa husika iandae muhtasari wa kikao cha utendaji cha
chama cha mkoa wa kupitisha maamuzi hayo, MoU (makubaliano rasmi)
yasainiwe kati ya chama cha mkoa na kituo husika na hati hiyo nakala
yake iletwe TFF.
MoU hiyo ionyeshe majukumu ya chama cha mpira
cha mkoa kama kutoa vifaa, kutoa mwalimu, usimamizi nk na pia kuonyesha
majukumu ya mwenye kituo kama kutoa uwanja,ulinzi nk. MoU itaonyesha
pia nani atafaidika na vipaji vitakavyoibuliwa kati ya mzazi,kituo na
chama cha mkoa.
TFF itaandaa MoU ya mfano kwa ajili ya vyama vyote
vya mikoa na ingependa kufikia tarehe 31/Desemba/2015 kila mkoa uwe
umetekeleza jambo hilo.
No comments:
Post a Comment