Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kinachodhaminiwa na
bia ya Kilimanjaro Premium Lager kimeanza mazoezi leo asubuhi katika
uwanja wa Boko Veterani kujiandaa na mchezo wa marudaino kuwania kufuzu
kwa CHAN dhidi ya uganda mwishoni mwa wiki ijayo.
Stars inayonolewa
na makocha wazawa, Charles Mkwasa na msaidizi wake Hemded Morocco,
itakua ikifanya mazoezi asubuhi na jioni katika uwanja huo wa Boko
Veterani, huku timu ikiweka kambi yake katika hoteli ya Kiromo mjini
Bagamoyo.
Wachezaji wote walioitwa wameripoti kambini tangu jana na
leo wamefanya mazoezi asubuhi isipokua Aggrey Morris ambaye ni majeruhi
nafasi yake imekuchukuliwa na Vicent Andrew (Mtibwa Sugar) na Jonas
Mkude aliyekwenda kufanya majaribio Afrika Kusini nafasi yake ikizibwa
na Mudathir Yahya (Azam FC).
No comments:
Post a Comment