Shirika
la polisi wa kimataifa Interpol limesema linasimamisha uhusiano wake na
FIFA uliokuwa na lengo la kuchunguza na kukabiliana na visa vya
upangwaji wa matokeo ya mechi za kandanda, kutokana na kashfa ya rushwa
inayolizonga shirikisho hilo la soka duniani.
Miaka minne
iliyopita FIFA iliipa interpol dolla millioni 22 kufadhili mradi ulio na
lengo la kuendeleza maadili katika secta ya michezo.Interpol inasema washirika wake wote ni sharti wadumishe na kuendeleze maadili na taratibu zinazotumiwa na interpol katika utendaji kazi wake.
FIFA imesema imesikitishwa na uamuzi huo wa Interpol na kuongeza kuwa mradi huo wa mikakati ya kuzua udandanyifu katika soka hauhusiani kwa vyovyote vile na kashfa ya madai ya rushwa dhidi ya FIFA.
No comments:
Post a Comment