Kiungo
wa kati wa Arsenal Abou Diaby ni miongoni mwa wachezaji wa Arsenal
wanaoondoka katika kilabu hiyo baada ya Arsenal kuchapisha majina ya
wachezaji wake walioachiliwa na klabu hiyo msimu huu.
Diaby
anaungana katika orodha hiyo na beki wa Aston Villa Ron Vlaar ambaye
kilabu hiyo bado inajaribu kuafikiana naye mkataba mpya na Wes Brown
ambaye kandarasi yake imekamilika katika klabu ya Sunderland.Chelsea nayo inamtoa Didier Drogba ikiwa ni mchezaji wa pakee anayeondoka kilabu hiyo kwa uhamisho wa bure huku klabu ya Hull City pia ikiwatoa wachezaji wake 13 akiwemo Mayonor Figueroa,Paul McShane na Yannick Sagbo.
No comments:
Post a Comment