Stars ambayo
jana jioni ilipoteza mchezo wake wa mwisho dhidi ya Lesotho baada ya
kufungwa bao 1-0, imerejea baadaa ya kupoteza michezo yote mitatu ya
kundi B, baada ya kufungwa na Swaziland, Madagascar na Lesotho.
Mara baada ya
mchezo wa jana dhidi ya Lesotho, kocha mkuu wa Taifa Stars Mart Nooij
alisema amesikitishwa na matokeo ya timu yake katika hatua hiyo ya awali
baada ya kupoteza michezo yote mitatu.
Nooij alisema,
mpira wa miguu umebadilika kwani matarajio yake yamekua tofauti, kwani
kiwango walivyoonyesha wapinzani wake katika kundi B vimemstajaabisha.
“Mpira wa sasa
hautazami nani yupo juu katika renki za FIFA, tulikua na matarajio ya
kufanya vizuri katika michuano hii lakini baada ya dakika ya 90 za kila
mchezo matokeo hayakua mazuri kwetu” alisema Nooij”
Kuhusu kufuzu
kwa AFCON 2017, Nooij amesema katika kikosi chake alichokwenda nacho
Cosafa alikua na wachezaji saba aliowapandisha, anaamini wamepata
uzoefu, na sasa atawajumuisha na wachezaji ambao hawakuweza kushiriki
michuano hiyo kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri.
Taifa Stars
inatarajia kucheza kucheza mchezo wake wa kwanza wa kuwania kufuzu kwa
AFCON 2017 dhidi ya Misri, tarehe 14 Juni 2015 katika uwanja wa Borg el
Arab jijini Alexandria.
No comments:
Post a Comment