Kocha ‘mpya’ wa Azam FC, Stewart Hall anaratajia kuanza kazi anatarajia kuanza Juni 15, mwaka huu.
Hall anayereja Azam FC kwa mara ya tatu ndani ya kipindi cha miaka sita, ameingia mkataba wa miaka miwili kuinoa Azam Fc.
Msemaji wa Azam FC, Jaffar Idd Maganga amethibitisha kuhusiana na hilo na kusema atasaidiwa na kocha wa makipa kutoka England.
“Ataanza kazi tarehe 15 mwezi ujao, kwa sasa unaweza kusema tayari ni kocha wa Azam FC,” alisema.
“Tumeingia naye mkataba wa miaka miwili, tunaaamini atakuwa msaada mkubwa kwa kuwa tayari anaijua Azam FC na nini inataka.”
Huo unakuwa mkataba wa tatu Hall raia wa Uingereza anaingia na timu hiyo waliokuwa mabingwa wa Tanzania kabla ya kuvuliwa ubingwa huo msimu uliopita na Yanga ya Dar es Salaam
Kwa hisani ya Saleh Jembe blog
No comments:
Post a Comment