Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, May 28, 2015

DIAMOND PLATINUM BALOZI WA MZIIKI


NYOTA wa muziki wa bongo flava nchini Diamond Platinumz amewataka wasanii wa Tanzania kusambaza nyimbo zao kwa njia ya teknolojia ili kunufaika na jasho lao. 


Diamond aliyasema hayo wakati akizindua teknolojia ya Mziiki ili kuziingiza sokoni kazi zake baada ya kushauriana na wadau anaoshirikiana nao kikazi ambayo pia yeye ni balozi anayeitangaza
”Tanzania ina wanamuziki wengi wenye vipaji lakini wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi ambazo zimekuwa zikiwafanya wasifike mbali zaidi ya muziki wao kusikika hapa nchini na wengi wao kutamba kwa muda mfupi na kupotea katika ulimwengu hivyo watumie teknolojia hii kupeleka kazi zao sokoni ili kujikwamua”,  alisema Diamond
Amesema sababu kubwa iliyomsukuma kufanya biashara ya muziki kupitia progamu hii ni kwamba nyimbo zake ziweze kuwafikia washabiki wake popote na muda wowote kwa urahisi kupitia simu zao za mkononi na anakuwa na uhakika wa kupata mapato tofauti na zinavyosambazwa na wasambazaji wa mtaani. 

“Duniani kuna ushindani katika nyanja zote  hivyo sisi wanamuziki wa Tanzania tunapaswa kuhakikisha tunatoa muziki wa viwango vya juu kuhakikisha tunalenga zaidi katika masoko ya ndani na nje kama wenzetu wanavyofanya kusambaza kazi zao kupitia kampuni zinazotumia teknolojia ya kisasa na kumnufaisha msanii kama ilivyo program hii ya Mziiki. Kuna umuhimu mkubwa wa kujiamini, kufanya vizuri ili tuweze kutangaza Tanzania, kutangaza lugha ya Kiswahili na kupata mapato ya kutosha kutokana na kazi ya muziki ambayo ikifanywa kitaalamu inalipa kwa kiasi kikubwa” anasema Diamond


Programu ya Mziiki ambayo ilizinduliwa na Vodacom kwa kushirikiana na Spice VAS Africa imeanza kufanya kazi na wanamuziki wa hapa nchini na nje ya nchi na katika kipindi cha muda mfupi tayari imesajili wanamuziki wapatao 1,000 ambao kazi zao hususani zile mpya zitasambazwa kwa njia ya kidigitali na malengo yake makubwa ni kuhakikisha wanamuziki wanapeleka kazi zao sokoni kwa haraka na kunufaika na jasho lao ambapo wananchi wengi wanaotumia mtandao kwenye simu zao kupakua nyimbo wazipendazo za wanamuziki ambao wamejiunga kwenye tovuti ya kampuni hiyo ambayo inapatikana kwa kubofya tovuti ya www.mziiki.com.

No comments:

Post a Comment