|
Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa wakazi wa mkoa wa
shinyanga,mikoa yote kanda ya ziwa na mashabiki wetu wote walioko nchi nzima na
sehemu mbalimbali duniani kwa kutoa ushirikiano wao wa dhati kwetu katika
michezo yetu ya ligi kuu tanzania bara msimu wa mwaka 2014-2015 iliomalizika
tarehe 9/05/2015.
Tunasema asanteni sana kwa michango yenu ya hali na mali,kifedha,kimawazo na
ushauri pia,na hasa katika kipindi kigumu ambacho tumepitia.
ulikuwa ni msimu wetu wa kwanza kushiriki katika ligi mengi tumejifunza na
kuona mazuri na magumu katika ligi hii na soka la tanzania kwa ujumla,tunaahidi
kuiandaa timu kwa wakati muafaka na kwa weledi mkubwa lengo likiwa ni kufanya
vizuri zaidi katika msimu ujao wa ligi kuu Tanzania Bara.
Tunasisitiza kuwa bado hatujaanza kushughurika na swala la usajili wa mchezaji
kwasasa na wala hatujafanya mazungumza na mchezaji yoyotekuhusu kumsajili,
tunasubiri ripoti ya mwalimu wetu Mathias Rule kujua anapendekeza tufanye nini
katika kuboresha timu yetu.
Tunakanusha vikali Taarifa ambazo zinasambaa hivi sasa kuwa
tunafanya au tumefanya mazungumzo na baadhi ya wachezaji ili
kuwasajili akiwemo Juma Kaseja na Beki wa mtibwa sugar Salim Mbonde
hatuna mazungumzo na wachezaji hao na hatutafanya usajili wowote bila kupata
ripoti ya mwalimu.
kama ripoti ya mwalimu itaelekeza tufanye usajili tutafanya hivyo na uongozi
umejipanga kufanya usajili wenye tija na umakini wa kutosha kwa manufaa ya timu
yetu ya Stand United fc.
Imetolewa na Idara ya Habari Stand United Fc.
Isaac Edward
Afisa habari.
0759 11 34 54
Bottom of Form
|
No comments:
Post a Comment