Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, May 30, 2015

RIO FERDINAND ASTAAFU SOKA.

Nahodha wa zamani wa England, Rio Ferdinand, ameamua kustaafu Soka.
Ferdinand, mwenye Miaka 36, alimpoteza Mkewe Rebecca aliezaa nae Watoto Watatu hapo Mei Mosi Mwaka huu baada kuugua kansa na kufariki.
Katika maisha yake ya Soka aliichezea Timu ya Taifa ya England mara 81 na pia kuwa Nahodha wake.
Kwenye Klabu, Ferdinand alizichezea West Ham, Leeds United, Man United na kumalizia Msimu huu akiwa QPR ambayo imeshushwa Daraja toka Ligi Kuu England.
Akiwa na Man United, Ferdinand alitwaa Ubingwa wa England mara kadhaa na pia UEFA CHAMPIONS LIGI pamoja na Klabu Bingwa ya Dunia.
Akitangaza kustaafu, Ferdinand alitoa shukran kwa Mameneja na Wafanyakazi wa Klabu alizopitia pamoja na Familia yake na hasa Mkewe.
Ferdinand akisherekea Ubingwa akiwa na Klabu ya  Manchester United mwaka  2003 Kwenye Ubingwa wa Ligi Kuu England akiwa na  David Beckham kwenye picha.

Ferdinand akipeana mkono  na Kaka yake  Anton walipokutana Uso kwa uso na  Manchester United dhidi ya West Ham huko Upton Park mnamo mwaka 2005.


Siyo tu kwenye Ushindi Rio Ferdinand pia alipokuwa akiukosa ushindi Aliumia na hapa walitolewa nje England kwenye Kombe la Dunia

Cristiano Ronaldo mwezi wa tano mwaka  2007 huko  Old Trafford walipoutwaa ubingwa na hapa Ferdinand alipata picha ya pamoja.

Ferdinand akiwa na  Joe Cole mwaka 2008 hukoM oscow

Nemanja Vidic, Anderson, Patrice Evra, Edwin van der Sar, Carlos Tevez, Ferdinand, Brown, Ryan Giggs na Mikael Silvestre wakishangilia baada ya kuitwanga Chelsea huko Moscow mnamo mwaka 2008

Ferdinand akipozi na  Ferguson pamoja na  Giggs na Makombe yao mwaka 2008
2009
Manchester United kwenye picha ya pamoja mwaka  2009 walipoibuka na Ubingwa.Rio akiwa na Moyes na Nemanja Vidic
Mwali!!Rio akishangilia moja ya bao lake akiwa Old TraffordKwenye Chumba cha kubadilishia nguo Rio akiendesha Shangwe za nguvu akiwa UnitedUbingwa wa Uefa Champions
Mavuno!! Ligi Kuu na Klabu BingwaKwenye Tofauti!NBA 2013

No comments:

Post a Comment