ABEL HERNANDEZ AFUNGIWA MECHI 3 KWA KOSA LA KUMPIGA NGUMI BEKI WA UNITED PHIL JONES.
FA,
Chama cha Soka England, Leo hii kimethibitisha kufungiwa Mechi 3 kwa
Mchezaji wa Hull City Timu iliyoshuka Daraja toka Ligi Kuu England, Abel Hernandez,
kwa kumpiga ngumi Beki wa Man United, Phil Jones, katika Dakika ya 70
ya Mechi ya mwisho ya Ligi Kuu England ambayo ilimalizika 0-0 na
kuthibitisha Hull kushuka Daraja baada ya Newcastle kuicharaza West Ham
2-0 na kunusurika kushuka. Tukio hilo la ngumi ya Hernandez
halikuonwa na Refa lakini lilinaswa kwenye Video na FA kumfungulia
Mashitaka na Mchezaji huyo kutoka Uruguay kukiri kosa na sasa atatumikia
adhabu yake Msimu ujao akiwa Daraja la chini la Championship.
No comments:
Post a Comment