Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, April 17, 2015

ZIFF YATANGAZA FILAMU ZITAZOSHINDANIA TUZO YA SEMBENE OUSMANE


Tamasha la ZIFF limetangaza filamu 16 zitakazoshindana katika kugombea tuzo ya Sembene Ousmane katika tamasha litakalofanyika baadaye mwaka huu. Filamu zinatoka katika nchi 11 ambazo ni pamoja na Marekani, Brazil, Senegal, Madagascar, Ghana, Cameroon, Morocco, Kenya, South Africa, Ethiopia and Tanzania.
“Shindano hili limetungwa ili kuboresha ufundi wa kutengeneza filamu fupi zinazobuniwa na vijana wa Kiafrika”, alisema Fabrizio Colombo, Mkurugenzi Msaidiziwa ZIFF. “Filamu 16 zimo katika kinyang’anyiro hicho, na washindi watatu watapewa $2000 kila mmoja ili kuwasaidia kutengeneza filamu nyingine tayari kwa tamasha la ZIFF mwaka ujao” aliongezea.
Bernd Multhaup washirika la GIZ, wadhaminiwatuzohii, alinakiliwa akisema, “Tuliamuwa kutoa zawadi tatu ili kuwapa motisha watengeneza filamu wengi zaidi kwa kupitia tuzo ya Sembene. Tunatambua kuwa filamu fupi zinauwezo mkubwa wa kuboresha ubunifu bila ya kupunguza ubora wa filamu”.
Hao washindi watatu watatakiwa kutuma hadithi zao pamoja na mpango-kazi wautengenezaji wa hizo filamu kabla hawajapewa fedha walizoshinda ilikuhakikisha filamu zitatengenezwa kuwahi tamasha lijalo mwakani. Kwa njia hiyo ZIFF itahakikisha kupata filamu nyingine na kuboresha ufundi wa kutengeneza filamu fupi na bora.
Filamu 16 zilizochaguliwani:
Lesley: Victor Okoye Frank, USA / 15 min
O Canto da Iona: Thiago B. Mendonca, Brazil / 25 min
Maruna: Molly Kane, Senegal / 15 min
Aisaa’s Story: Iquo B Essien, USA / 15 min
Madama Esther: Luck Razanajaona, Madagascar / 15 min
The Traveller: Victoria Dogbe, Ghana / 9 min
Damaru: AgborObed, Cameroon / 24 min
Houkak: YounesYoufsi, Morocco / 17 min
Kwaku: Anthony Nti, Ghana / 16 min
SamakiMchangani: AmilShivji, Tanzania, 30min
Kilimo 2: Neema& Warren Reed, Tanzania / 6 min
LiberteEmprisonnee: Sara Mikayel, Senegal /16min
SokoSonko: EkwaMsangi, Kenya / 22 min
Uthando: TulananaBohela, South Africa, 20min
Grandma Knows Best: Tamara Dawit, Ethiopia, 16min
Vitrin, Regis Talia, Cameroon, 15min
JuuYaMradi:Mradi huu unadhaminiwa na GIZ,shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ujerumani ambalo linasaidia Tanzania na Jumuiaya Afrika Mashariki. ZIFF ni tamasha kubwa kuliko yote Afrika mashariki na ambalo linatambuliwa kimataifa. Tamasha linadhaminiwa na ZUKU kupitia mkataba waudhamini wa miaka 10 utaoisha 2021.

No comments:

Post a Comment