Chama cha
soka mkoa wa Dar es salaam (DRFA), kimetangaza zawadi kwa washindi wa michuano ya ligi
ya wanawake mkoa wa Dar es salaam inayoendelea katika viwanja mbalimbali
Jijini.
Mwenyekiti
wa chama hicho Almas Kasongo,amesema zawadi hizo zitatolewa kwa mshindi wa
kwanza na wapili,mchezaji bora wa mashindano,mfungaji bora,kipa bora,timu yenye
nidhamu na mwamuzi bora.
Mshindi wa
kwanza atazawadiwa Kikombe,jezi seti moja
na kiasi cha shilingi milioni moja na laki tano (1,500,000/=),Mshindi wa
pili atapata jezi seti moja na kiasi cha shilingi laki saba (700,000/=)
,Mchezaji bora wa mashindano atazawadiwa kiasi cha shilingi laki mbili
(200,000/=),Mfungaji bora atapata shilingi laki moja na nusu (150,000/=),Kipa
bora atapata shilingi laki moja na nusu (150,000/=),Timu yenye nidhamu
itazawadiwa shilingi laki nne (400,000/=),huku mwamuzi bora akiondoka na
shilingi laki mbili (200,000/=).
Ligi hiyo
yenye jumla ya timu 8 imeanza kutimua vumbi jumapili ya April 19/2015,kwa
mchezo wa ufunguzi uliozikuwanisha timu za Temeke Squad dhidi ya Ever-Green
Queens,na kushuhudiwa Ever-Green ikichomoza na ushindi wa kishindo wa mabao
5-1,yaliyofungwa na Sherida Boniface dakika ya 7,19na 39,na mengine yakifungwa
na Donicia Daniel katika dakika ya 60 na 65,na lile la kufutia machozi kwa
Temeke Squad likifungwa na Aisha Juma.
Tumi zote
zinzoshiriki michuano hiyo ya ligi ya wanawako mkoa wa Dar es salaam ni pamoja
na
IMETOLEWA NA DRFA,
Omary Katanga Mkuu Wa Habari Na
Mawasiliano,DRFA
No comments:
Post a Comment