Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, March 30, 2015

MZIZIMA MOTORSPORTS CLUB WAJA NA SPRINT RALLY APRILI 12, BAGAMYO

Dereva Frank Taylor akijaribu gari lake aina ya VX Landscuiser kwenye eneo la Kingani, Bagamoyo ambalo litafanyika mbio za zilizoandaliwa na Mzizizma Motorsports Club ya jijini Dar es Salaam, Aprili mwaka huu.








UONGOZI wa Mzizima Motorsports Club (MMSC) umeandaa mashindano ya mbio za magari yatakayofanyika Aprili 12 mjini Bagamoyo, Pwani.

Akizungumza jijini Katibu Mkuu wa Mzizima Motorsports Club, Hidaya Kambanga alisema kuwa mashindano  hayo yatakuwa ya umbali wa kilometa moja na yatahusisha waendasha, baiskeli, pikipiki na magari.

“Mashindano haya yatakuwa yanahusisha waendasha baiskeli, pikipiki na magari ya aina zote kwenye umbali wa kilometa moja lengo likiwa ni kuhamasisha madereva mbio za magari badala ya kukimbizana barabarani kwani usalama unakuwa mdogo”, alisema Hidaya.

Pia alisema madareva watakaopenda kushiriki wanatakiwa kulipa ada ya 20,000 na wadereva ambao wanaruhusiwa ni wale wenye umri wa miaka 19 na kuendelea.
Hidaya alisema zaidi ya madereva 150 wanatarajiwa kushiriki na kuwaomba wengine ambao wanapenda kushiriki kujisajili na kulipa ada.

Naye Mshauri wa mambo ya ufundi wa Mzizima, Athman Hamisi alisema madereva wote wanatakiwa kuja na kofia ngumu (element), kizima moto (fire extinguisher) na akasisitiza kabla ya kuwasha gari kuanza mbio watahakikisha kila dereva amefunga mkanda kw ajili ya usalama.

Pia alisema dereva ambaye atakuja akiwa amekunywa kilevi chochote ataruhusiwa kuingia kwenye mashindano.

Mashindano hayo ya Mbio yamedhaminiwa na Redbull, Majipoa, grassroots sports and events na National Rally Company (NRC)

No comments:

Post a Comment