Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, March 26, 2015

MARTIN SKRTEL NA STEVEN GERRARD KUKOSA MECHI TATU

FA, Chama cha Soka England, kimemfungia Sentahafu wa Liverpool Martin Skrtel Mechi 3 baada ya kumpata na hatia ya kumkanyaga kwa makusudi Kipa wa Manchester United David De Gea Jumapili iliyopita Uwanjani Anfield wakati wa Mechi Ligi Kuu England ambayo Liverpool walichapwa 2-1.

Tukio hilo ambalo lilitokea karibu na mwisho wa Mechi hiyo halikuonwa na Refa Martin Atkinson lakini lilinaswa kwenye Video ambayo ilipitiwa na Jopo Huru la FA la Marefa wa zamani Watatu na wote kuafiki kuwa lilikuwa Kosa linalostahili Kadi Nyekundu na hapo ndipo FA iliamua kumshitaki.
Skrtel, Mchezaji wa Kimataifa wa Slovakia mwenye Miaka 30, alikana Shitaka lake hapo Jana kwa kujitetea alimkanyaga De Gea kwa bahati mbaya.
Lakini hii Leo Jopo Huru la FA limetupilia mbali utetezi wa Sentahafu huyo na kumfungia Mechi 3 na atazikosa Mechi 2 za Ligi Kuu England za Aprili 4 huko Emirates na Arsenal na ile ya Anfield na Newcastle hapo Aprili 14 na Marudiano ya FA CUP ya Robo Fainali huko Ewood Park na Blackburn Rovers hapo Aprili 8.

Hizo pia ndizo Mechi ambazo Kepteni Steven Gerrard atazikosa baada ya Kadi Nyekundu kwenye Mechi hiyo hiyo aliyolambwa Sekunde 38 tu tangu aingie Uwanjani kutoka Benchi kwa kumkanyaga kwa kusudi Ander Herrera wa Man United.

No comments:

Post a Comment