Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, March 28, 2015

MALAWI YAWASILI MWANZA

Timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) tayari imewasili leo jijini Mwanza majira ya saa sita mchana, ikiwa na kikosi chake kamili kwa ajili ya mchezo dhidi ya Taifa Stars siku ya jumapili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Malawi imewasili ikiwa na kikosi chake kamili cha wachezaji 18 na kufikia katika hotel ya JB Belimonte, wakiwemo wachezaji saba wanaocheza soka la kulipwa katika nchi za Afrika Kusini, Congo DR, Msumbuji na Zimbabwe.

Wachezaji wa kimataifa waliowasili ni nahodha Joseph Kamwendo (TP Mazembe -Congo DR), Chimango Kayira (Costal de Soul - Msumbiji), Frank Banda (HBC Songo - Msumbiji), Esau Kanyenda (Polokwane City - Afrika Kusini),  Harry Nyirenda (Black Leopards - Afrika Kusini), Limbikani Mzava (Celtic - Afrika Kusini) Gerald Phiri (Caps United - Zimbambwe)

Wegine ni McDonald Harawa (Hoyale FC), Richard Chipuwa (Wanderers), Lucky Malata (Silver), John Lanjesi (Civo), Francis Mulimbika (Wanderers), John Banda (Blue Eagle), Earnest Tambwe (Surestream) , Micium Mhone (Blue Eagle), Chikoti Chiriwa (Red Lions), Peter Wadabwa (Silver) na Amos Khamula(Support Ballaton).

Mkuu wa msafara ni Alexander Waya, Kocha mkuu Young Chimodzi, kocha msaidizi Jack Chamangwana, kocha wa makipa Pillip Nyasulu, Daktari wa timu Levison Mwale, Meneja wa timu Frank Ndawa na Afisa Habari James Sangala.

Kikosi cha timu ya Taifa ya Malawi kinatarajiwa kufanya mazoezi leo saa 10 jioni katika uwanja wa CCM Kirumba, huku siku ya jumamosi wakipata nafasi ya kufanya mazoezi tena kwenye uwanja huo wa mchezo.

Kesho jumamosi saa 5 kamili asubuhi kutafanyika mkutano na waandishi wa habari katika hoteli ya La Kairo iliyopo Kirumba jijini Mwanza, kocha wa Stars Mart Nooij na kocha wa The Flames Young Chimodzi wataongelea maandilizi ya mchezo wao wa siku  ya jumapili.

No comments:

Post a Comment