MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii kupitia Mradi wake wa
Kituo cha Mpira wa Miguu kijulikanacho kama NSSF-REAL MADRID Sports Academy
wameanza usajili wa kusaka vijana wenye vipaji watakao jiunga na kituo hicho
kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi wa
Operesheni wa NSSF, Crescentius Magori alisema kuwa anashukuru wazazi kwa
kujitokeza kwa wingi kwenye uandikishaji wa kuwabaini vijana ambapo wana vipaji
vya mpira wa miguu.
“Uandikishaji huu
utahusisha vijana wa kiume waliozaliwa kati ya 2001 hadi 2002 June, na
unafanyika bure kuanzia leo (jana) na
kesho na utaendelea wiki ijayo siku ya jumamosi na jumapili kuanzia saa maoja
asubuhi hadi saa tisa aliasiri”, alisema Magori.
Zoezi la kuandikisha halina gharama zozote bali kila mmoja
atatakiwakuja na picha mbili za passport size na cheti cha kuzaliwa na mzazi
wake au mlezi wake ili kujaza fomu maalum ambayo atapewa namba ya ushiriki.
Pia Magori alisema kuwa vijana ambao watachaguliwa kujiunga
na kituo chao pamoja na kufundishwa soka pia watakuwa wnaafundishwa masomo ya
elimu ya sekondari kulingana na mtaala wa elimu ya Tanzania ili wawe wazuri
katika soka na kichwani pia.
Zoezi hili linalengo
la kupata vijana 500 ambao watakaofanyiwa majaribio na wataalamu kutoka Klabu
ya Real Madrid na hatimaye kupatikana vijana 30 amabo ndio wataingia katika
shule maalum ya mafunzo kwa awamu ya kwanza.
Shirika la NSSF linatoa wito kwa vijana kujitokeza kwani ni
fursa kwao ya kuweza kujiendeleza kimichezo na kujiajiri kupitia michezo.
Mkurugenzi wa Operesheni wa NSSF, Crescentius Magori akizungumza na baadhi ya wasimamizi wa zoezi la usaili |
Mkurugenzi wa Operesheni wa NSSF, Crescentius Magori (KULIA) akiteta jambo na mwakilishi wa Real Madrid (kushoto) wakati usajili ukiendelea |
No comments:
Post a Comment