Timu ya Taifa ya Tanzania ya mpira wa miguu (Taifa Stars Maboresho) leo inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya kombani ya jiji la Tanga katika Uwanja wa Mkwakwani.
Mchezo huo wa kujipima
nguvu ni sehemu ya program ya kocha mkuu Mart Nooj ya kupata nafasi ya kuona
maendeleo ya wachezaji wake ambao anawaandaa kuwa wachezaji wa timu ya Taifa ya
baadae.
Mara baada ya mechi ya
leo jioni jijini Tanga, timu hiyo itarejea jijini Dar es salaam ili kutoa fursa
kwa wachezaji kujiunga na vilabu vyao kwa ajili ya michezo inayowakabili
mwishoni mwa wiki ikiwemo Ligi Kuu ya Vodacom na Fainali ya Ligi Daraja la
Kwanza.
No comments:
Post a Comment