Timu
za taifa za kriketi kutoka nchi za Kenya, Uganda na Namibia zitawasili
Tanzania Alhamisi hii kwa ajili ya michuani ya ligi ya ICC-Afrika
Division 1 kwa wavulana chini ya miaka 19 itakayoanza Jumapili Dar es
Salaam.
Kwa mujibu wa Nasser, maofisa wasimamizi wa michuano hiyo kutoka Afrika ya Kusini na Namibia pia watawasili mapema kabla ya mashindano kuanza.
“Maandalizi yote yamekamilika na tumejiandaa kuzipokea timu zinazowasili kwa ajili ya kukaa Dar es Salaam kwa muda wa juma moja”, alisema Nasser.
Timu itakayokuwa bingwa itafaulu kucheza kombe la dunia la vijana chini ya miaka 19 kwa wavulana itakayofanyika mwakani, Dhaka, Bangladeshi.
Waandaaji wa michuano hiyo mikubwa, Chama cha Kriketi Africa (ACA),chenye makao yake makuu chini Afrika ya Kusini katika mji wa Benoni, tayari wametoa ratiba ambapo wenyeji Tanzania watacheza na Namibia siku ya Jumapili katika moja ya mechi za ufunguzi itakayofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu Cha Dar esn Salaam (UDSM).
Mechi nyingine zitakazochezwa siku ya ufunguzi (Jumapili ni kama ifuatavyo.
Kenya vs Nigeria- Uwanja wa Gymkhana Dar es Salaam.
Uganda vs Botswana- Uwanja wa Annadil Burhan.i
Michuano hiyo itachezwa katika ova 50.
Kwa hisani ya BBC
No comments:
Post a Comment