Timu ya Taifa ya Tanzania ya mpira wa ufukweni
(beach soccer) inatarajia kurusha karata yake ya kwanza Jumapili kwa kucheza na
Kenya katika raundi ya kwanza ya michuano ya Afrika kwa ajili ya fainali za
Afrika za michuano hiyo zitakazofanyika Aprili mwaka huu nchini Shelisheli.
Mchezo huo utachezwa Mombasa nchini Kenya
na mchezo wa marudiano utachezwa nchini kati ya Februari 20 na 22 mwaka huu
Akizungumza jijini, Kocha wa timu hiyo
John Mwansasu, alisema maandalizi ya kwa ajili ya mchezo huo yanaendelea vema
na wamecheza michezo miwili ya kirafiki na timu ya Zanzibar na kusema walipoteza
mmoja na kushinda mmoja.
“Maandalizi yanaendelea na kiwango cha
wachezaji kinaimarika kila siku na nawaahidi watanzania kurudi na ushindi japo
sikupata michezo ya kirafiki ya kimataifa lakini nina imani na timu yangu”,
alisema Mwansasu.
Kocha John Mwansasu anasaidiwa na Ali
Shariff 'Adolf' kutoka Zanzibar, na Meneja wa timu ni George Lucas na kikosi
cha timu ya Taifa ya Tanzania ya mpira wa ufukweni (beach soccer) kinaundwa na
wachezaji 15, saba toka Zanzibar na nane
Tanzania bara
Iwapo timu ya Tanzania itasonga mbele,
katika raundi ya pili itacheza na Misri ikianzia nyumbani kati ya Machi 13 na
15 mwaka huu.
Timu hiyo inayofanya mazoezi kwenye ufukwe
wa Escape One inatarajiwa kuondoka nchini Ijumaa ya wiki hii.
No comments:
Post a Comment