Kiungo wa timu ya Coastal Union,
John Mahundi amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Disemba 2014 wa Ligi Kuu
ya Vodacom (VPL) inayoendelea kutimua vumbi kwenye viwanja mbalimbali nchini.
Mahundi alitoa mchango mkubwa kwa
timu yake ya Coastal Union mwezi Disemba mwaka jana na kuchaguliwa na jopo la
makocha linalofanya kazi ya kuchagua mchezaji bora wa kila mwezi.
Aidha mshambuliaji wa timu ya
Polisi Morogoro, Said Bahanuzi amechaguliwa kuwa mchezaji bora mwezi Januari
2015 wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoendelea kutimua vumbi mzunguko wa 15
kwenye viwanja mbalimbali nchini.
Bahanuzi anayechezea timu ya
Polisi Morogoro kwa mkopo akitokea timu ya Young Africans amekua na mchango
mkubwa kwa timu yake tangu kujiunga nayo mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya
Vodacom nchini.
Kwa kuibuka wachezaji bora, Mahundi
na Bahanuzi watazawadiwa fedha taslimu sh. milioni moja kwa kila mmoja kutoka
kwa wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.
No comments:
Post a Comment