Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, February 18, 2015

AFRICAN SPORTS NA MWADUI KUTAFUTA BINGWA LIGI DARAJA LA KWANZA JUMAPILI UWANJA WA TAIFA





TIMU  za African Sports  ya Tanga na Mwadui FC ya Shinyanga zinatarajiwa kucheza mchezo wa fainali   kusaka Bingwa wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) siku ya  Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

 African Sports waliibuka washindi wa kwanza katika Kundi A, na Mwadui FC washindi wa kwanza Kundi B watacheza mchezo huo wa fainali ambapo Bingwa atapewa zawadi ya Kombe na medali, hali kadhalika kwa msindi wa pili.

 Akizungumza na waandishi wa habari jana Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Baraka Kizuguto alisema kwa mujibu wa Kanuni, ni lazima apatikane mshindi mmoja ambaye ni bingwa.

“Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ilimalizika mwishoni mwa wiki kwa timu nne kupanda Ligi Kuu kwa kila kundi kutoa timu mbili, Kundi A ni African Sports na Majimaji FC, Kundi B ni timu za Mwadui FC na Toto Africans,”alisema.

Alisema  timu za Green Worriors na Villa Squad zimeteremka  Daraja la pili baada ya kushika nafasi za mwisho kwenye msimamo wa Ligi Daraja la Kwanza, Villa Squad kutoka Kundi A na Green Warriors Kundi B.

Katika hatua nyingine, Rais wa TFF  Jamal Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa Wenyekiti wa klabu ya African Sports (Tanga) , Majimaji (Ruvuma),  Mwadui (Shinyanga) na Toto Africans ya Mwanza kwa timu zao kupanda Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).

 Katika salamu zake  Malinzi alisema klabu hizo zinapaswa kujipanga na kufanya maandalizi kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom 2015/2016, kwani VPL ni ngumu kutokana na timu zote kuwa na ushindani mkubwa wa kutafuta matokeo mazuri kuepeuka kushuka daraja.

 Kwa niaba ya TFF, familia ya mpira na watanzania kwa ujumla wanawapa pongezi timu za African Sports, Majimaji, Mwadui na Toto Africans kwa kupanda Ligi Kuu ya Vodacom na kuwatakia maandalizi mema ya VPL 2015/2016,”alisema.

No comments:

Post a Comment