Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, February 18, 2015

MAANDALIZI YA MIAKA 15 YA TAMASHA LA PASAKA,BAISKELI 100 KUTOLEWA KWA WALEMAVU MIKOA KUMI


Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari wakati akielezea maendeleo ya maandalizi ya miaka 15 tangu kuanzishwa kwa tamasha la Pasaka, sherehe ambazo zitafanyika wakati wa sikukuu ya Pasaka jijini Dar es salaam na kisha mikoani, Akizungumza katika mkutano huo Msama amesema mwaka huu tamasha la pasaka ni maalum kwa Msama Promotion imepanga kuwanunulia baiskeli 100 za walemavu ambazo zitagawanywa katika mikoa 10 hapa nchini.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akifafanua zaidi kwa waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi ya miaka 15 tangu kuanzishwa kwa tamasha la Pasaka, na pia sherehe hizo zitaambatana na utoaji wa baiskeli 100 za walemavu ambazo zitagawanywa katika mikoa 10 hapa nchini.
Msama ameongeza kuwa hivi sasa wako katika mazungumzo na waimbaji wa muziki wa injili kutoka nje ya nchi hasa kule Afrika Kusini na Uingereza, waimbaji ambao wako katika mazungumza na kampuni ya Msama Promotion ni Solomon Mahlangu, Rebecca Malope, Keke Pofolo na wengine wote kutoka nchini Afrika Kusini.
Msama alisema kuwa idadi ya mikoa ambayo imeomba iandae onesho la miaka 15 ya Tamasha la Pasaka sasa imefikia 17,amesema Tamasha la Pasaka kwa mwaka huu litakuwa la aina yake tangu walipoanzisha tamasha lao mwaka 2000.

“Tumepokea maombi ya wadau kutoka mikoa 17 wakitaka tupeleke Tamasha la Pasaka mikoani kwao. Tunachofanya kwenye kamati yangu ni kupokea maoni kwa njia mbalimbali kwa wadau wetu wa huko.
“Lakini si kupendekezwa au kuombwa tu na wadau ndiyo kigezo cha kupewa nafasi, lazima tuangalie na mazingira ya mkoa husika katika mambo ya matamasha,” alisema Msama.Aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Morogoro, Rukwa, Mara, Singida, Arusha, Ruvuma, Mbeya, Iringa, Tanga, Dar s Salaam, Mtwara, Mwanza, Dodoma, Tabora, Shinyanga, Kilimanjaro na Zanzibar.

Alisema kamati yake inatarajia kukutana Jumatano wiki hii na kufanya tathmini ya maombi kwa wadau wao wa maeneo hayo ili kupata mikoa sahihi ambayo tamasha hilo litafanyika mwaka huu.
Tamasha la Pasaka linaandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es Salaam, ambayo pia huandaa Tamasha la Krismas kila mwaka, lakini wanataka Tamasha la Pasaka mwaka huu liwe bora zaidi kwa sababu wanasherehekea miaka 15 tangu waanzishe tamasha hilo.

No comments:

Post a Comment