CHAMA cha
Soka Mkoa wa Ilala (IDFA) kimemteua Mwandishi wa Michezo wa Kampuni ya Magazeti
ya Serikali(TSN) inayozalisha
Habarileo, Spotileo na Dailynews Rahel
Pallangyo kuwa Kocha wa timu ya wanawake
Ilala.
Akizungumza
na gazeti hili jana Katibu Mkuu wa IDFA Daudi Kanuti alisema Pallangyo kwa
kushirikiana na makocha wengine wa Ilala watasaidiana kuinoa timu hiyo kwa
ajili ya michuano ya kombe la taifa ya wanawake inayoendelea.
Alisema
wamemteua Pallangyo kwa ajili ya mashindano hayo ya taifa ambaye ana leseni C
ya ukocha ili kufanyia kazi cheti chake.
“Tunaamini
tukiwapa nafasi makocha wanawake wataonyesha uwezo, na kwa vile tayari ana
leseni tumempa nafasi kuifanyia kazi, asiwe kabatini kiendelee
kuharibika,”alisema.
Kwa upande
wa Pallangyo alisema anafurahi kupata fursa hiyo na anaahidi kuonyesha uwezo
wake kwa vitendo.
“Naahidi
kutumia taaluma yangu kuonyesha watu kwamba hata makocha wanawake wakipewa
nafasi wanaweza kufanya mambo makubwa ili kuondoa dhana kwa jamii kuwa wanaume
pekee ndio wanaoweza,”alisema
Mtihani wa
kwanza kwa Pallangyo itakuwa katika mchezo wa kwanza wa robo fainali
utakaochezwa kesho jioni kati ya Ilala dhidi ya Mtwara utakaochezwa Karume.
Ilala,
Kindoni na Temeke ziliingia moja kwa moja kwenye raundi ya pili ya fainali hizo
No comments:
Post a Comment