SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeanza ukarabati katika Uwanja wa Kaitaba uliopo mkoani Kagera kuanzia Januari 12,2015.
Rais
wa TFF, Jamal Malinzi alisema kuwa kutokana na ukarabati huo tayari
Kagera Sugar imeshaomba kutumia Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kwa ajili
ya mechi zake za nyumbani. Katika hatua nyingine, Malinzi alisema
kutokana na kikao cha Kamati ya Utendaji cha FIFA kilichokutana hivi
karibuni kiliweka wazi kila Mwanachama wa FIFA ataendelea kupata dola za
kimalekani 600,000 kwa mwaka kwa ajili ya maendeleo ya Soka.
Muonekano wa Uwanja wa mpira wa Kaitaba Stadium wa Bukoba baada ya kuanza ukarabati huo.
Ukarabati
huu wa Uwanja wa Kaitaba umeifanya mechi ya Kagera Sugar na Mbeya City
kuhamishiwa kwenye Jiji la Mwanza na utachezwa siku ya Jumamosi tarehe
17.01.2015 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.
Kwa
mujibu wa Rais wa TFF, Jamal Malinzi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama
cha Soka Mkoa wa Kagera,watakutana na uongozi wa klabu ya Kagera Sugar
ili kufahamu watatumia uwanja upi kwenye mechi zao za nyumbani za Ligi
Kuu.
Kagera italazimika kuhamisha na kucheza nje ya mkoa huo mechi zake
zote za Ligi Kuu hadi hapo uwanja huo wa Kaitaba utakapokamilika .
TFF
tayari ilishatangaza kuwa mechi kati ya Kagera na Mbeya City,itachezwa
kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza,uwanja ambao ni mzuri na uko jirani
na Mkoa wa Kagera.
Kuhamishiwa kwa mechi za Ligi Kuu kwenye uwanja wa CCM Kirumba ni faraja
kwa wapenzi,washabiki na wadau wa soka hapa,baada ya kuikosa kwa muda
mrefu,tangu Toto ishuke daraja msumu uliopita. Kaitaba ni miongoni mwa
viwanja ambayo vimekuwa vilalamikiwa kutokana na kuwa na mabonde na
miinuko ,hivyo kuwekewa nyasi bandia kutaondoa malalamiko yaliyokuwa
yakitolewa na baadhi ya timu zilizokuwa zikiutumia kucheza na Kagera
Sugar .
Mbali na Kaitaba,mwingine ambao uko kwenye ukarabati wa kuwekewa nyasi
bandia ni uwanja mkongwe wa Nyamagana wa Jiji la Mwanza, ambao uko
katika hatua za mwisho ili kuwekewa zuria la nyasi hizo.
Picha na Faustine Ruta, Bukoba
Taswira ya Uwanja wa kaitaba hii leo Jumatatu 12 januari 2015 unavyoonekana baada ya kuanza ukarabati huo.
No comments:
Post a Comment