Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, January 8, 2015

COPA DEL REY: ATLETICO MADRID 2 vs 0 REAL MADRID, RAUL GARCIA NA JOSE GIMENEZ WAIPA USHINDI ATLETICO KWENYE DABI YAO EL DERBI MADRILENO

Wachezaji wa Atletico Madrid wakipongezana na kushangilia baada ya kuipiga bao 2-0 Mahasimu wao wakubwa kwenye Uwanja Vicente Calderon  Dabi ya Jiji la Madrid, maarufu kama El Derbi madrileño kwenye mechi yao ya kwanza ya Copa Del Rey. Ronaldo alianzia Benchi Real ikimuanzisha Bale ambaye hakuweza kufurukuta lolote na Ronaldo kushindwa pia kutamba.
Raul Garcia akishangilia bao lake la kwanza kwa Atletico Madrid usiku huu kwenye mchezo wa Copa Del Rey Atletico Madrid.
BAO zote mbili zimefungwa katika kipindi cha pili, Bao la kwanza ni la mkwaju wa penati wa Raúl García dakika ya 58 na bao la pili ni la kichwa la José Giménez dakika ya 76 kipindi cha pili na Mtanange kumalizika kwa 2-0 dhidi ya Real Madrid.
Raul Garcia akiachia shuti kali la mkwaju wa penati na kufanya 1-0 dhidi ya Real madrid.Ronaldo(kulia) alianzia nje kwenye BenchiAlijionea laivu timu yake ikifungwa bao la kwanza la mkwaju wa penati..Dabi ya Jiji la Madrid, maarufu kama El Derbi madrileño, kati ya Atletico Madrid na Real Madrid hakuna aliyeliona lango la mwenzake katika kipindi cha kwanza timu zote mbili zilikimaliza kipindi hicha cha dakika 45 kwa 0-0.Torres akituliza mpiraTorres na mpira!Makocha timu zote mbili wakipongezana..kabla ya kipute kuannza..Torres kuanza mchezo huu wa kukata na shoka!Usiku huu ni Dabi, Mtanange  Uwanjani Vicente Calderon itakapopigwa Dabi ya Jiji la Madrid, maarufu kama El Derbi madrileño, kati ya Atletico Madrid na Real Madrid.
Real Madrid ndio Mabingwa Watetezi wa Kombe hili ambapo kwenye Fainali Mwezi Mei Mwaka Jana waliibwaga FC Barcelona.
Kwenye Raundi hii, Barcelona wao wataanza Nyumbani Nou Camp na mpinzani wao ni Elche.

Mechi za Copa del Rey huchezwa kwa mtindo wa nje ndani, yaani Nyumbani na Ugenini na Marudiano ya Raundi hii yataanza Januari 13.



RATIBA:Usiku huu 
Jumatano Januari 7
22:00 Villarreal CF v Real Sociedad
23:00 Atletico de Madrid v Real Madrid CF
00:01 Valencia C.F v RCD Espanyol
00:01 UD Almeria v Getafe CF

Alhamisi Januari 8
22:00 Granada CF v Sevilla FC
00:01 FC Barcelona v Elche CF

No comments:

Post a Comment