Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, December 11, 2014

KOCHA WA ZAMANI MAN UNITED MIKE PHELAN AMLAUMU VAN GAAL KWA JANGA LA MAJERUHI

Kocha wa zamani wa Man United Mike PhelanKwenye Miezi Mitano ya Msimu huu mpya Manchester United imekumbwa na matukio ya Majeruhi kwa Wachezaji wake mara 43 na kuzipita Klabu nyingine zote za Ligi Kuu England na hili limemfanya Kocha wa zamani wa Klabu hiyo kwenye himaya ya Sir Alex Ferguson, Mike Phelan, anyooshe kidole kwa jinsi uongozi wa Meneja mpya Louis van Gaal unavyowafanyisha Mazoezi Wachezaji wao.

Phelan amesema: “Wameleta Watu wapya wenye mtazamo mpya na kumweka pembeni Tony Strudwick ambae ndie alikuwa Mkufunzi wa Mazoezi na aliemjua kila Mchezaji wa United nje ndani.”
Phelan, mwenye Miaka 52, ndie aliekuwa Meneja Msaidizi chini ya Sir Alex Ferguson kwa Miaka Mitano na hivi sasa ni Kocha wa Timu ya Kwanza huko Norwich City.

Kocha huyo amesema mtindo na mfumo mpya wa Mazoezi huenda ndio ulisababisha kina Michael Carrick, Phil Jones, Rafael na Radamel Falcao kuwa nje kwa kipindi kirefu wakiwa na maumivu.
Phelan ameeleza: “Kinachotokea ni Wachezaji wale wale kuumia kila mara na ni lazima utafute sababu. Nadhani ni tatizo la kubadili mfumo wa Mazoezi.”

No comments:

Post a Comment