Kamati ya Mpira wa Miguu wa Vijana ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeunda jopo la watu watano
kuhakiki umri wa wachezaji watakaoshiriki hatua ya ngazi ya Taifa ya michuano
ya Copa Coca-Cola 2014.
Michuano hiyo ya ngazi ya Taifa
itafanyika Dar es Salaam kuanzia Desemba 13 hadi 20 mwaka huu. Uhakiki wa umri
utafanyika Desemba 11 na 12 mwaka huu wakati timu zote zinatakiwa kuwasili
Shule ya Filbert Bayi mkoani Pwani kuanzia Desemba 10 mwaka huu.
Jopo hilo la uhakiki linaongozwa na
Mkufunzi wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Henry Tandau.
Wengine katika jopo hilo ni Ally Mayay, Charles Boniface Mkwasa, Dk. Jonas
Tiboroha na Richard Yomba.
Timu 16 zitakazocheza michuano hiyo
inayoshirikisha watoto wenye umri chini ya miaka 15 ni Arusha, Dodoma, Geita,
Katavi, Kigoma, Kinondoni, Kusini Pemba, Kusini Unguja, Lindi, Mbeya, Mjini
Magharibi, Morogoro, Mwanza, Ruvuma, Simiyu na Tanga.
Vyama vya mpira wa miguu vya mikoa
vinakumbushwa kutuma TFF fomu za usajili ambazo zinatakiwa kuambatanishwa vyeti
vya kuzaliwa vya wachezaji husika.
No comments:
Post a Comment