Kikosi cha wachezaji 23 wa Taifa Stars tayari
kimewasili Johannesburg, Afrika Kusini tayari kwa maandalizi ya mechi dhidi ya
Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya Swaziland.
Mechi hiyo itafanyika Jumapili (Novemba
16 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa wa Somhlolo jijini Swaziland. Taifa Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwepo Johannesburg hadi Ijumaa
itakapoondoka kwenda Mbabane.
Wachezaji wote walioitwa na Kocha Mart
Nooij wapo kwenye msafara huo isipokuwa kiungo mshambuliaji Mrisho Ngasa ambaye
amebaki Dar es Salaam kutokana na matatizo ya kifamilia.
Taifa Stars inatarajia kurejea nyumbani
Jumatatu (Novemba 17 mwaka huu) saa 12.45 jioni kwa ndege ya South Africa
Airways.
Wakati huo huo, kikosi cha
maboresho cha Taifa Stars kitacheza mechi ya kirafiki na timu ya Taifa ya
Rwanda kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 23. Mechi hiyo itachezwa Desemba
9 mwaka huu nchini Tanzania.
Kikosi cha maboresho cha Taifa Stars
kinachoundwa na wachezaji wenye umri chini ya miaka 23 kitakuwa kinakutana mara
moja kila mwezi hadi Mei mwakani kwa ajili ya mazoezi na kucheza mechi moja ya
kirafiki.
Kocha Mart Nooij atatangaza kikosi kwa
ajili ya mechi hiyo na programu nzima mara atakaporejea kutoka Swaziland.
No comments:
Post a Comment