Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, November 7, 2014

SURE BOY KUKABIDHIWA ZAWADI YAKE KESHO


Salum Abubakar1

Mchezaji bora wa VPL kwa mwezi Oktoba, Salum Abubakar wa Azam atakabidhiwa zawadi yake kesho (Novemba 8 mwaka huu) kabla ya mechi kati ya Azam na Coastal Union.
Abubakar ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) aliwashinda wachezaji wengine 20, huku wanne kati ya hao wakichuana naye kwa karibu.
Wachezaji hao ni Joseph Mahundi wa Coastal Union, Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Rashid Mandawa (Kagera Sugar) na Najim Magulu wa JKT Ruvu Stars.
Kwa kuibuka mchezaji bora, Abubakar atazawadiwa kikombe na fedha taslimu sh. milioni moja kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.
Jopo maalumu la makocha waliopo katika viwanja vyote vinavyotumika kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ndiyo wanaofanya kazi ya kuchagua mchezaji bora kwa kila mechi kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa, na baadaye alama zao kujumlishwa ili kumpata mshindi wa mwezi.

No comments:

Post a Comment