BRENDAN RODGERS AKERWA NA BALOTELLI KUBADILISHANA JEZI NA PEPE WAKATI WA MAPUMZIKO JANA.! WAKIAMBULIA KIPIGO CHA BAO 3-0 KUTOKA KWA REAL!
Kocha wa Liverpool Brendan Mario
Balotelli sasa anakabiliwa na kisago toka kwa Meneja wake Brendan
Rodgers kwa kubadilishana Jezi na Sentahafu wa Real Madrid Pepe wakati
wa Haftaimu wa Mechi iliyochezwa Anfield Jumatano Usiku na Liverpool
kutandikwa 3-0.
Akiteta na Pepe na baadae kupeana jeziMipango ya Jezi ilianzia hapa kwenye stori za hapa na pale wakitoka nje ya Uwanja kwenda kupumzikaNipe jezi!Wakati
huo wa Mapumziko Liverpool ilikuwa tayari iko nyuma kwa hizo Bao 3-0
zilizofungwa na Cristiano Ronaldo na mbili za Karim Benzema huku Mario
Balotelli akizunguka tu Uwanjani na kubadilishwa kabla Kipindi cha Pili
kuanza na nafasi yake kuchukuliwa na Adam Lallana. Akiongea kuhusu
tukio hilo la Balotelli kubadilishana Jezi, Rodgers alisema: “Ni kitu
ambacho sikikubali. Kama unataka kufanya hivyo, fanya mwisho wa Mechi.
Nitalishughulikia suala hili Alhamisi.” Msimu
uliopita tukio kama hilo lilitokea huko Stamford Bridge Liverpool
walipocheza na Chelsea na Beki wao Mamadou Sakho kubadilishana Jezi na
aliekuwa Straika wa Chelsea Samuel Eto'o na kumuudhi Brendan Rodgers
ambae Jana alilikumbushia na kusema walilishughulikia ndani ya Klabu. Mbali
ya kugubikwa na tukio hili la kubadilishana Jezi, Balotelli hivi sasa
anasakamwa kwa uchezaji duni huko Liverpool lakini Meneja Rodgers
amesema Jana alimtoa wakati wa Haftaimu ili kubadili mbinu tu. Brendan
Rodgers ameeleza: “Ni mbinu tu. Nilidhani tunahitaji nguvu na wepesi
zaidi kwenye Kiungo na nilitaka Mtu mwepesi kuwahangaisha Masentahafu
wao na niliona Raheem Sterling anaweza hilo. Adam Lallana aliingia
kuleta uhai kwenye Kiungo na alifanya bidii sana.”Karim Benzema akishangilia moja ya bao zake Aaaah!!
No comments:
Post a Comment