


Hii ni mara ya kwanza kwa Real kuifunga Liverpool katika Mashindano ya Ulaya baada ya kufungwa Mechi zao zote 3 walizokutana huko nyuma na ni Cristiano Ronaldo ndie aliefungua milango kwa kutengeneza na yeye mwenyewe kupachika Bao la kifundi baada ya kucheza ‘moja mbili’ na James Rodriguez kwenye Dakika ya 23.

Bao la tatu lilifungwa na Karim Benzema tena baada ya kupigwa kona na Pepe kujitwisha kichwa kwenye eneo hatari ndani ya box na hatimae Karim Benzema kuupata na kuusindikiza langoni mwa Liverpool na kumfunga kipa Mignolet na kufanya 3-0 katika dakika ya 41.




No comments:
Post a Comment