
Valdes, mwenye Miaka 32, aliumia Goti hilo Mwezi Machi na kulikosa Kombe la Dunia kuichezea Nchi yake Spain.
Kabla ya kuumia, Valdes alikuwa ameshatoa uamuzi wa kuondoka Barcelona mwishoni mwa Msimu uliopita baada ya kukataa kuongeza Mkataba wake uliokuwa ukimalizika.

Inasemekana Meneja wa Man United, Louis van Gaal, ndie aliemkaribisha Valdes kufanya Mazoezi na Klabu yake wakati akiendelea kujiweka fiti baada ya kupona.

Taarifa kutoka Man United ilisema: “Valdes atakuwa chini ya uangalizi wa Madaktari wa Manchester United akiendelea kupona Goti lake wakati akisubiri kuanza Mazoezi na Timu ya Kwanza.”
Hata hivyo, Man United, ambae Kipa wake wa kwanza ni Mhispania David De Gea na Nambari mbili ni Anders Lindegaard, haijapasua kama itampa Mkataba Valdes.
No comments:
Post a Comment