Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, September 12, 2014

RATIBA LIGI KUU ENGLAND, JUMAMOSI SEPT.13.2014, ARSENAL vs MANCHESTER CITY. JUMAPILI NI OLD TRAFFORD MAN UNITED vs QPR


Ligi kuu England, inarejea tena Jumamosi baada ya kupisha Mechi za Kimataifa kwa Wiki mbili na Mechi ya kwanza kabisa ipo Emirates na hii ni Bigi Mechi kati ya Arsenal na Manchester City ambao ndio Mabingwa Watetezi.
Mwezi uliopita, Arsenal iliichapa Man City Bao 3-0 Uwanjani Wembley kwenye Mechi ya kufungua pazia Msimu mpya kugombea Ngao ya Hisani lakini kwenye Ligi Arsenal wameshinda Mechi moja na kutoka Sare Mechi 2 zilizopita.
Nao Man City walianza kwa ushindi katika Mechi mbili za kwanza lakini kwenye Mechi yao ya mwisho Uwanjani kwao Etihad walitandikwa 1-0 na Stoke City.

Mbali ya Mechi hii, Chelsea, ambao wanaongoza Ligi kwa kushinda Mechi zao zote 3, watakuwa kwao Stamford Bridge kucheza na Swansea City ambao ndio wamefungana nao kileleni na ambao pia wameshinda Mechi zao zote 3.
Lakini Chelsea huenda wakamkosa Straika wao Diego Costa ambae
ndie amewafungia Bao 4 katika Mechi 3 kwani Mchezaji huyo ana matatizo ya Mguu.

LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:

Jumamosi Septemba 13
14:45 Arsenal v Man City
17:00 Chelsea v Swansea
17:00 Crystal Palace v Burnley
17:00 Southampton v Newcastle
17:00 Stoke v Leicester
17:00 Sunderland v Tottenham
17:00 West Brom v Everton
19:30 Liverpool v Aston Villa
Jumapili Septemba 14
18:00 Man United v QPR
Jumatatu Septemba 15
22:00 Hull v West Ham

No comments:

Post a Comment