Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, September 12, 2014

PISTORIUS AKUTWA NA HATIA YA KUMUUA MPENZI WAKE BILA KUKUSUDIA LAKINI ANAWEZA KWENDA JELA



Oscar Pistorius akiwasili katika mahakama ya Pretoria leo mchana kusikiliza kesi inayomkalibi
JAJI anayeendesha kesi ya mauaji inayomhusu mwanariadha wa Afrika kusini, Oscar Pistorius, hajamkuta na hatia ya kumuua kwa kukusudia mpenzi wake, mwanariadha wa Olympic, Reeva Steenkamp
Katika kesi hiyo iliyosikilizwa leo, Jaji Thokozile Masipa alisema ushahidi wa kuthibitisha kuwa Pistorius, 27 aliua kwa makusudi haujajitosheleza kutoka kwa mwendesha mashitaka.
"Ushahidi wa kuhusika na mauaji, huo umejitosheleza" alisema Jaji, lakini hakutoa hukumu juu ya kesi hiyo ya Pistorius na kutoa wito kwa ajili ya chakula cha mchana mahakamani hapo.
Mbivu na mbichi zitajulikana leo hii.


Oscar Pistorius alisema alimuua Reeva Steenkamp bila kukusudia katika siku ya wapendanao 'Valentine Day' mwaka 2013.
Hata kama Pistorius hatakutwa na hatia ya kuua kwa kukusudia, bado anaweza kwenda jela kwa kosa la kumuua Steenkamp.
Mwanaridha huyo alikiri kutenda kosa hilo, lakini alisema hakukusudia.
Mashahidi wa utetezi walidai kuwa Pistorius alimuua kwa makusudi mpenzi wake kutokana na ugomvi uliotokea baina yao na majirani walisikia.


Mama yake Reeva Steenkamp, June (kulia), akiwa mahakamani hapo leo alhamisi

No comments:

Post a Comment