Winga
wa Simba Uhuru Selemani amesema kwasasa anajisikia faraja na kujiona ni
mwenye amani zaidi tangu kurejea kwa kocha Mzambia Patrick Phiri.
Akiongea
na Rockersports Uhuru amesema Phiri kwake ni kama mzazi ambaye amekuwa
akimpa nasaha mara kwa mara na kumrejesha mchezoni kisaikolojia jambo
ambalo anamini litamfanya sasa kucheza soka kwa kiwango chake tofauti na
misimu miwili iliyopita.
Akiongea
kwa masikitiko Uhuru amesema ilifika wakati alikata tamaa kabisa ya
kucheza mpira kwa kiwango cha juu kutokana na kukosa nafasi katika
kikosi cha Simba na hata thamani yake kushuka ndani ya wekundu hao wa
Msimbazi.
Amesema
tangu kurejea kwa Phiri mambo yamebadilika kwakuwa kocha huyo ameanza
kumuamini tena na sasa anacheza mpira wake ule ule wa zamani.
"nashukuru
mungu Phiri ni kama mzazi kwangu ananishauri mambo mengi ya ndani na
nje ya mpira naona mabadiliko katika uchezaji wangu wa mpira" amesema
Uhuru.
Ameendelea
kusema "hapo nyuma nilikata tamaa kutokana na hata viongozi walikuwa
hawanithamini hasa baada ya kuumia goti na nilipoelekea India kufanyiwa
upasuaji lakini sasa najiamini na ninacheza mpira, kwahiyo namuona Phiri
kama mzazi wangu"
Rockersports
ilifanya mahojiano maalum na kocha Phiri juu ya uwezo wa Uhuru wa Uhuru
Selemani ambaye alimsifia winga huyo kwa kusema kwasasa amerejea na
kwamba anamtegemea kubadilisha hali ya mchezo uwanjani kwa kuwani
anamtumia kama mchezaji huru anapokuwa uwanjani.
"uhuru
ni mchezaji huru uwanjani ni mzuri anapokuwa anaingia tunapokuwa
tumeshindwa plan ya kwanza namtegemea sana kikosini hasa tunapokuwa
tunataka kuwachanganya wapinzani"
Uhuru
Selemani alirejea Simba akitokea Coastal Union ya Tanga kabla ya kuanza
kwa mzunguko wa wa pili wa ligi msimu uliopita kuanza.
Kabla
ya kujiunga na Coastal alikuwa akiichezea Azam fc ambako alihamia kwa
mkopo akitokea Simba ambayo ilimuacha kutokana na kutokuwa fiti kwa
aslimia mia moja baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti nchini India.
No comments:
Post a Comment