Klabu ya Manchester United imekamilisha usajili wake kwa kumsajili Radamel Falcao ambaye amejiunga kwa mkopo wa msimu mzima.
Falcao alijiunga na Monaco kwa dau la dola milioni hamsini mwaka 2013.
Baadhi waliona taarifa hizo kama fununu tu.
Bila shaka usajili wa Falcao katika Manchester
United unaonekana kama mapinduzi kwani vilabu vingi vilikuwa vimemuotea
Falcao ambaye anachezea klabu ya Ufaransa ya Monaco.
Falcao ameifungia Monaco jumla ya mabao 11 akicheza michezo 20. Mkataba huo unaipa fursa Manchester United kumnunua
mchezaji huyo kwa pauni milioni 43.5 mwishoni wa kipindi cha mkopo.
Klabu ya Louis van Gaal ambayo kama vilabu
vingine Ulaya vilifahamu tu kumhusu mchezaji huyo na uwezo wa kununua
katika dakika za mwisho mwisho.
Wakati huohuo, Manchester United itaikopesha Real Madrid mchezaji wake nyota Javier Hernandez.
Mshambuliaji
huyu alikuwa akihusishwa na kuelekea Manchester City katika siku ya
mwisho ambapo pia Arsenal wiki iliyopita walijaribu kujiunga na mbio
hizo.
Lakini
United ikatupia chambo bora katika ndoano na kufanikiwa kupata saini
yake ambapo sasa hofu ya majeruhi ya Robin van Persie haitakuwa na
wasiwasi mkubwa huku pia wakiwa wanaelekea kumuuza Danny Welbeck na
Javier Hernandez ambaye amejiunga na Real Madrid.
No comments:
Post a Comment