Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) inatarajia kuondoka nchini Ijumaa (Agosti 29 mwaka huu) kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya mechi ya kirafiki na timu ya Taifa ya nchi hiyo (Banyana Banyana).
Twiga Stars inakwenda huko kwa mwaliko wa Chama cha Mpira wa Miguu
Afrika Kusini (SAFA) kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Jumapili
(Agosti 31 mwaka huu) katika mji wa Polokwane.
Msafara wa timu hiyo utaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Saloum ambapo utajumuisha
wachezaji 18 na benchi la ufundi lenye watu watano.
Wachezaji kwenye msafara huo ni Amina Bilali, Anastaz Katunzi, Asha
Rashid, Donisia Minja, Esther Chabruma, Etoe Mlenzi, Fatuma Jawadu,
Fatuma Makusanya, Fatuma Maonya, Fatuma Swaleh, Happiness Mwaipaja,
Maimuna Said, Mwajuma Abdillahi, Mwanahamis Shurua, Shelda Mafuru,
Sophia Mwasikili, Therese Yona na Zena Rashid.
Benchi la Ufundi linaongozwa na Kocha Rogasian Kaijage, na msaidizi
wake Nasra Mohamed. Wengine ni Christine Luambano (daktari), Furaha
Mnele (Meneja) na Mwanahamisi Nyomi (mtunza vifaa).
Timu hiyo inatarajia kurejea nchini Septemba 2 mwaka huu kwa ndege ya Fastjet.
No comments:
Post a Comment