Kikosi cha Stars |
Taifa Stars sasa itacheza na Burundi katika mechi ya kalenda ya
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) badala ya Morocco
iliyokuwa icheze nayo awali kuamua kufuta mechi hiyo baada ya kushindwa
kuwapata wachezaji wake wa kulipwa.
Mechi dhidi ya Burundi itachezwa Septemba 6 mwaka huu jijini
Bujumbura, na kikosi cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro
Premium Lager kinaingia kambini Jumapili (Agosti 31 mwaka huu) mchana
jijini Dar es Salaam.
Wachezaji 26 walioitwa na Kocha Mkuu Mart Nooij kwa ajili ya mechi
hiyo ni makipa Deogratias Munishi (Yanga) na Mwadini Ali (Azam). Mabeki
Said Morad (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Shomari Kapombe (Azam), Nadir
Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Aggrey Morris (Azam), Joram
Mgeveke (Simba) na Charles Edward (Yanga).
Viungo ni Erasto Nyoni (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar),
Amri Kiemba (Simba), Himid Mao (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said
Ndemla (Simba), Said Juma (Yanga) na Haruna Chanongo (Simba).
Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Khamis Mcha (Azam), Simon Msuva
(Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC), Mbwana Samata (TP Mazembe,
DRC), Mrisho Ngassa (Yanga), Mwegane Yeya (Mbeya City) na Juma Liuzio
(ZESCO, Zambia).
No comments:
Post a Comment