Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) wameandaa kozi ya
ukufunzi wa utawala itakayofanyika Desemba mwaka huu.
Kozi hiyo itakayoendeshwa na wakufunzi kutoka FIFA itafanyika jijini
Dar es Salaam kuanzia Desemba 1 hadi 5 mwaka huu, ambapo sifa ya chini
ya elimu kwa wanaotaka kushiriki ni kidato cha nne.
Kwa wanaotaka kushiriki kozi hiyo wanatakiwa kutuma maombi yao kwa
Katibu Mkuu wa TFF. Mwisho wa kupokea maombi hayo ni Septemba 5 mwaka
huu ambapo wanatakiwa pia kuwasilisha nakala za vyeti vyao vya
kitaaluma.
MTIHANI WA WAAMUZI, MAKAMISHNA SEPTEMBA 5
Mtihani wa utimamu wa mwili (physical fitness test) kwa waamuzi wanaotaka kuchezesha mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu huu utafanyika katika vituo viwili kuanzia Septemba 5-6 mwaka huu.
Mtihani wa utimamu wa mwili (physical fitness test) kwa waamuzi wanaotaka kuchezesha mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu huu utafanyika katika vituo viwili kuanzia Septemba 5-6 mwaka huu.
Waamuzi watakaoshiriki mtihani huo ni wenye beji za Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na wale wa class one. Pia kutakuwa na
semina wa makamishna wanaotaka kusimamia mechi za VPL na FDL ambayo
itafanyika Septemba 7 mwaka huu.
Vituo vya mtihani huo ni Dar es Salaam na Shinyanga. Kituo cha Dar es
Salaam ni kwa waamuzi na makamishna kutoka mikoa ya Dar es Salaam,
Dodoma, Iringa, Kilimanjaro, Lindi, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Njombe,
Pwani, Ruvuma na Tanga.
Kituo cha Shinyanga ni kwa waamuzi na makamishna kutoka mikoa ya
Arusha, Geita, Kagera, Katavi, Kigoma, Manyara, Mara, Mwanza, Rukwa,
Shinyanga, Simiyu, Singida na Tabora.
Waamuzi wote ambao wamechezesha VPL na FDL msimu wa 2013/2014 na
kupata matatizo au kuondolewa kwenye ligi hawahusiki na mtihani huo.
Washiriki wanatakiwa kufika kituoni siku moja kabla.
Wasimamizi ni Charles Ndagala, Israel Mujuni, Issarow Chacha, Joan
Minja, Pascal Chiganga, Riziki Majala, Said Nassoro, Salum Chama, Soud
Abdi, Victor Mwandike na Zahara Mohamed.
No comments:
Post a Comment