Katibu mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa |
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeongeza kwa saa 48
muda wa kufanya usajili wa wachezaji kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom
(VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
Muda huo umeongezwa kutokana na matatizo ya mtandao yaliyojitokeza
kwa siku mbili hizi (Agosti 26 na 27 mwaka huu). Awali usajili ulikuwa
umalizike Agosti 27 mwaka huu, na sasa usajili utafungwa kesho (Agosti
29 mwaka huu) saa 6 usiku.
Hadi jana (Agosti 27 mwaka huu) saa 6 usiku ambao ulikuwa muda wa
mwisho ni timu ya Daraja la Kwanza ya Kimondo FC ya Mbeya iliyokuwa
imeingiza wachezaji wake wote kwenye system.
Kwa upande wa wachezaji kutoka nje ya Tanzania ambao wanahitaji Hati
ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) dirisha lao kwenye Mfumo wa Uhamisho wa
Wachezaji (TMS) wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)
litafungwa Septemba 6 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment