Emanuel Okwi wa Uganda ambaye msimu uliopita alikuwa anaichezea Yanga, akiwa na jezi namba 25 aliyokabidhiwa mara baada ya kusaini tena Simba baada ya kukachwa na Yanga katika usajili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inayotarajia kuanza mwezi ujao.
Kamati
ya usajili ya klabu Simba imetangaza kumsajili mshambuliaji wao wa
zamani Emmanuel Okwi ambaye msimu uliopita alikuwa kwa mahasimu wao wa
soka Yanga.
Akiongea mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu hiyo Zackaria Hans
Poppe amesema wamemsajili Okwi baada ya mshambuliaji huyo raia wa Uganga
kuomba kusajiliwa na klabu hiyo kufuatia kuvunjiwa mkataba na Yanga.
Poppe
amesema mkataba wa Okwi na Simba ni wa wazi kwani mchezaji huyo ambaye
amejiunga na Simba akiwa huru atakuwa huru kuondoka muda wowote atakapo
taka kufanya hivyo.
Okwi
anasajiliwa na Simba ikiwa siku mbili zimesalia kabla ya dirisha la
usajili wa wachezaji wa ndani halijafungwa huku usajili wa wachezaji
kutoka nje dirisha lake likitarajiwa kufungwa Septemba 6 2014
No comments:
Post a Comment