Douglas Costa (kulia) nafukuziwa na Manchester United na Arsenal |
Arsenal
na Manchester United wameambiwa waziwazi kuwa wanapaswa kupandisha dau
mpaka kufikia pauni milioni £40 endapo kweli wanataka kumsajili Douglas
Costa kutoka Shakhtar Donetsk.
Costa
mwenye umri wa miaka 23 amekuwa akihusishwa na kuondoka Shakhtar wiki
zijazo kufuatia kugomea kurejea Ukraine kwasababu ya matatizo ya
kisiasa.
Uwezo
wake aliouonyesha katika klabu ya Shakhtar umepelekea vilabu vingi
barani Ulaya vikiwemo Arsenal na AC Milan ambavyo vimekuwa vikipimana
ubavu kudaka saini ya Mbrazil huyo.
Taarifa
kupitia gazeti la Daily Stars zimearifu kuwa mashetani wekundu
watapaswa kuongeza dau lao mpaka kufikia pauni milioni £40 ili aweze
kutua Emirate Stadium msimu huu wa kiangazi huku mabosi wa klabu yake
wakisema mshambuliaji huyo ni bora zaidi ya mwenzake Hulk.
Mchezaji mwenyewe anataka zaidi kuelekea Arsenal kuliko kujiunga na United.
No comments:
Post a Comment